15 Novemba 2025 - 18:30
Walowezi wa Israel Wateketeza Msikiti katika Ukingo wa Magharibi

Wizara ya Awqaf (Wakfu) na Mambo ya Kidini imesema kuwa walowezi walivamia Msikiti wa Hajjah Hamidah uliopo Salfit, kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi, na kulitaja tukio hilo kuwa “jinai ya kinyama na shambulio la wazi dhidi ya hisia za Waislamu.”

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt as -ABNA- Walowezi wa Israel wameteketeza msikiti na kuandika maandishi ya chuki kwenye kuta zake katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, kwa mujibu wa mamlaka za Palestina. Tukio hili ni miongoni mwa mashambulizi mengi ya hivi karibuni yanayofanywa kwa ujasiri mkubwa dhidi ya Wapalestina.

Wizara ya Awqaf (Wakfu) na Mambo ya Kidini imesema kuwa walowezi walivamia Msikiti wa Hajjah Hamidah uliopo Salfit, kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi, na kulitaja tukio hilo kuwa “jinai ya kinyama na shambulio la wazi dhidi ya hisia za Waislamu.”

Taarifa ya wizara ilieleza kwamba: “Shambulio hilo limesababisha sehemu za msikiti kuungua moto na kupakwa maandishi ya kibaguzi na magenge ya walowezi, ambao wamekuwa wakitekeleza mashambulizi ya kila siku dhidi ya maeneo matakatifu ya Kiislamu na mali za wananchi, huku kukiwa na ongezeko la kimfumo katika kiwango na aina ya ukiukaji huu.”

Vilevile, Harakati ya Hamas, ikilaani tukio hilo, ilisema kuwa: “Wazayuni wamekiuka hisia za kidini za Waislamu, na hatua za haraka za kimataifa zinahitajika kuchukuliwa dhidi ya uhalifu na uchokozi kama huu.”

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha